ALHARAMAIN PROFESSIONAL COLLEGE

Alharamain Professional College ni Chuo cha elimu ya kati kilichojikita katika kutoa mafunzo ya kitaaluma kwa viwango vya kimataifa. USAJILI NI REG/BTP/143P NACTVET

Chuo hiki kimeanzishwa kwa lengo la kujenga jamii yenye maarifa, ujuzi na weledi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira la sasa na baadae. Kupitia mitaala iliyobuniwa kwa umakini na walimu waliobobea, Alharamain Professional College inajivunia kutoa elimu bora inayomwandaa mwanafunzi kuwa mtaalamu anayetegemewa katika sekta ya fedha, uchumi,mipango,habari na mawawasiliano.

Je unataka kujisajili sasa hivi? Bonyeza link hii ujaze fomu mtandaoni

MATUMIZI YA AKILI MNEMBA(Artificial Intelligence). Bonyeza ROBOTI hapo chini kwa msaada wakati wa masomo. Unauliza topic na maswali kila topic na utapata msaada

Chuo hiki kinatilia mkazo maadili, nidhamu, ubunifu na ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji, kikilenga kuandaa wahitimu walio tayari kuleta mabadiliko chanya katika jamii na taifa kwa ujumla. Alharamain Professional College inaamini kwamba elimu ni msingi wa maendeleo, na hivyo huwapa wanafunzi mazingira bora ya kujifunza yanayochochea ubunifu, tafiti na ushirikiano wa kitaaluma.

Kwa kushirikiana na wadau wa elimu na sekta binafsi, Alharamain Professional College imejipambanua kama jukwaa la kuzalisha wataalamu mahiri katika nyanja za biashara, habari na mawasiliano, uhasibu na utunzaji fedha, hivyo kuimarisha mchango wake katika ujenzi wa taifa lenye maendeleo endelevu.

Bonyeza link hii kuona kozi moja kwa moja mtandaoni

KOZI ZINAZOFUNDISHWA

1.DIPLOMA IN ACCOUNTING

2.CERTIFICATE IN ACCOUNTING

3.DIPLOMA IN JOURNALISM

4.CERTIFICATE IN JOURNALISM

5.SHORT COURSES IN COMPUTER APPLICATION

📘 Kozi ya Uhasibu (Accounting)

Kozi ya Uhasibu katika Alhamain Professional College inalenga kuwapa wanafunzi maarifa ya kina na ujuzi wa kiutendaji unaohitajika katika ulimwengu wa biashara na fedha. Kozi hii inawaandaa wanafunzi kuwa wataalamu wa kusimamia, kutathmini, na kuwasilisha taarifa sahihi za kifedha kwa matumizi ya taasisi, kampuni, na mashirika.

Mambo Muhimu Yanayofundishwa:

  • Misingi ya Uhasibu (Principles of Accounting)
  • Uhasibu wa kifedha na usimamizi (Financial and Management Accounting)
  • Tathmini ya taarifa za fedha (Financial Statement Analysis)
  • Ushuru na sheria za kodi (Taxation and Tax Law)
  • Bajeti na mipango ya kifedha (Budgeting and Financial Planning)
  • Teknolojia ya Uhasibu — matumizi ya programu kama Tally, QuickBooks, na Excel.
  • Maadili ya taaluma ya uhasibu na udhibiti wa ndani (Professional Ethics and Internal Controls)

Malengo ya Kozi:

  • Kuwezesha wanafunzi kuelewa misingi ya uhasibu na matumizi yake katika ulimwengu wa biashara.
  • Kuandaa wataalamu wanaoweza kuandaa, kutathmini na kusimamia taarifa za fedha kwa uwazi na uadilifu.
  • Kuwajengea uwezo wa kutumia mifumo ya kisasa ya kielektroniki katika uhasibu.

Fursa za Kazi:

  • Mhasibu (Accountant)
  • Mkaguzi wa Hesabu (Auditor)
  • Afisa wa Fedha (Finance Officer)
  • Mshauri wa Kodi (Tax Consultant)
  • Meneja wa Bajeti (Budget Analyst)

📰 Kozi ya Uandishi wa Habari (Journalism)

Kozi ya Uandishi wa Habari katika Alhamain Professional College inalenga kuwapa wanafunzi maarifa ya kitaaluma na ujuzi wa vitendo katika tasnia ya habari. Wanafunzi wanajifunza mbinu bora za ukusanyaji, uchambuzi, na uwasilishaji wa habari kwa njia ya maandishi, sauti, picha, na mitandao ya kijamii.

Mambo Muhimu Yanayofundishwa:

  • Misingi ya Uandishi wa Habari (Principles of Journalism)
  • Maadili ya Uandishi wa Habari (Media Ethics)
  • Uandishi wa Habari kwa Vyombo mbalimbali (Print, Radio, TV, na Digital)
  • Uhariri na uwasilishaji wa habari (Editing and News Presentation)
  • Upigaji picha wa habari na uandishi wa habari za picha (Photojournalism)
  • Uandishi wa Makala na Ripoti za Uchunguzi (Feature and Investigative Reporting)
  • Matumizi ya teknolojia ya kisasa kwenye habari — kamera, sauti, na programu za kuhariri.

Malengo ya Kozi:

  • Kukuza uwezo wa wanafunzi katika ukusanyaji na uwasilishaji wa habari kwa uadilifu na weledi.
  • Kuandaa waandishi wa habari wenye maarifa na stadi za kukidhi mahitaji ya vyombo vya habari vya kisasa.
  • Kuwajengea wanafunzi mazoea ya kufuata maadili ya taaluma hii, kuandika kwa usahihi, kwa haraka, na kwa ukweli.

Fursa za Kazi:

  • Mwandishi wa Habari (Journalist/Reporter)
  • Mhariri wa Habari (News Editor)
  • Mtangazaji wa Redio au Televisheni (Radio/TV Presenter)
  • Mwandishi wa Makala (Feature Writer)
  • Mwandishi wa Habari za Mtandaoni (Digital Content Creator)
  • Mchambuzi wa Habari (News Analyst)

KARO

Karo kwa mwaka kila kozi ni sh.800,000. Utajitegemea Malazi na Chakula. Ukihitaji huduma ya hostel na chakula utalipia gharama zaidi

JISAJILI KIDIJITALI

Tupigie
× Karibu ALHARAMAIN